30 Mei 2024 - 17:02
Maandamano ya kuunga mkono Palestina yaendelea Ulaya licha ya ukandamizaji wa polisi

Kwa siku ya tatu mfululizo, Ufaransa inashuhudia maandamano makubwa ya kuunga mkono Palestina na kupinga mauaji ya kimbari yanayoendelezwa na utawala haramu wa Israel huko Gaza na pia mauaji ya hivi karibuni kabisa yaliyotekelezwa na utawal wa Israel huko Rafah.

Katika ripoti yake ya hivi punde siku ya Jumatano, Wizara ya Afya ya Palestina huko Gaza ilitangaza kuwa, tangu mwezi Oktoba utawala haramu wa Israel umeua Wapalestina 36,171 na kujeruhi 81,420 ambapo wengi ni wanawake na watoto.

Maandamano makubwa zaidi kufikia sasa yalifanyika mjini Paris siku ya Jumatano, ambapo maelfu walikusanyika katika Place Saint-Augustinm, wakitangaza mshikamano na Gaza kwa kusema, "Gaza…Paris iko pamoja nawe."

Waandamanaji pia walipiga nara dhidi ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa misimamo yake ya kuunga mkono utawala haramu wa Israel katika mauaji yake ya kimbari dhidi ya Wapalestina aktika Ukanda wa Gaza.

Vikosi vya polisi vya Ufaransa vimewashmbulia waandamanaji hao wa amani ili kuwatawanya, na kusababisha makabiliano makali kati ya pande mbili.

Nchini Uswidi, vikosi vya polisi vilitumia mbwa kuwashambulia wanafunzi wa Taasisi ya Kifalme ya Teknolojia huko Stockholm, walipokuwa wakipinga mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na Israel Gaza.Zaidi ya hayo, wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Ghent (UGent) nchini Ubelgiji walifanya maandamano ya kimya kuunga mkono Palestina na Gaza.

Mapema mwezi huu, Chuo Kikuu cha Ghent kilitangaza kuwa kinakata uhusiano na taasisi tatu za elimu za utawala wa Israel kutokana na jinai za utawala huo.

Nchini Uingerezxa waandamanaji walikusanyika nje ya Downing Street, makao makuu ya serikali ya Uingereza, kupinga uhalifu wa hivi karibuni wa kivita wa Israel.

Waandamanaji wanasema serikali ya Uingereza ni mshirika wa mauaji ya kimbari Gaza, kwa kutoa msaada wa kijeshi, kifedha, na kisiasa kwa utawala wa Kizayuni, msimamo ambao waandamanaji wanapinga lazima uachwe mara moja.


342/